Arsene Wenger aweka kandarasi ya miaka 2 Arsenal

Arsene Wenger akiinua kombe la FA aliloshinda baada ya kuichapa Chelsea 2-1 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsene Wenger akiinua kombe la FA aliloshinda baada ya kuichapa Chelsea 2-1

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger ametia saini kandarasi mpya ya miaka miwili katika klabu hiyo.

Mkataba huo hautahusisha kifungu cha kupumzika na utakapokamilika atakuwa ameiongoza klabu hiyo kwa miaka 23.

Mkataba huo huenda sio wa mwisho kulingana na pande zote mbili.

Arsenal ilimaliza katika nafasi ya tano msimu huu ,ikiwa ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo kumaliza miongoni mwa timu nne bora tangu mwaka 1996.

Walimaliza nyuma ya mabingwa wa ligi ya Uingereza Chelsea kwa pointi 18 lakini wakaiwashinda mabingwa hao 2-1 na kuchukua kombe la FA.

Wenger alikutana na mwenye klabu Stan Kroenke siku ya Jumatatu ili kutoa hatma yake, huku uamuzi huo ukitolewa kwa wakurugenzi wa bodi ya klabu hiyo na tangazo rasmi kutarajiwa siku ya Jumatano.