Utafiti wabaini uvutaji wa sigara huharibu maini ya vijusi

mwanamke mjamzito Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wataalam wa kisayansi walibaini kuwa kemikali za sigara huwaathiri vijusi wa kiume na wakike kwa njia tofauti

Athari za uvutaji wa sigara kwa watoto ambao hawajazaliwa zimetangazwa katika utafiti mpya kuhusu seli.

Wanasayansi wamebaini kwamba mchanganyiko wa kemikali zinazotengeneza siraga ni hatari hususan kwa seli za ini zinazokuwa.

Walibuni njia za kutambua athari za uvutaji wa sigara kwa wanawake wajawazito kwa nyama ya ini kwa kutumia seli za binadamu za urithi.

Jopo hilo la wataalam wa kisayansi likiongozwa na chuo kikuu cha Edinburgh, pia lilibaini kuwa kemikali za sigara huwaathiri vijusi wa kiume na wakike kwa njia tofauti.

Wakati wa utafiti wao walitumia seli zenye uwezo wa kubadilika na kuwa aina nyingine za seli - kutengeneza nyama la ini ya mtoto ambaye hajazaliwa.

Seli za ini ziliwekewa kemikali hatari zinazopatikana kwenye sigara, ukiwemo mchanganyiko unaojulikana kusambaa kwenye mwili wa kijusi wakati mama ,jamzito anapovuta sigara.

Utafiti huo ulibaini kuwa mchanganyiko wa kemikali - ambao ni sawa na ule uliopatikana kwenye sigara unaathiri ini la kijusi kuliko aina moja ya kemikali.

Athari ni za muda mrefu

Dkt. David Hay kutoka kituo cha dawa mbadala katika chuo kikuu cha Edinburgh anasema: "uvutaji wa sigara unafahamika kwa kuwa na mathara makubwa kwa vijusi,wakati tuna ukosefu wa zana zinazofaa za kufanyia utafiti suala hili kwa njia inayofaa zaidi.

Image caption Nyama za ini la kijusi cha kiume zilionekana kuwa na makovu huku mfumo mzima wa seli za ini la kijusi cha kike zikionekana kuharibika

Uvutaji wa sigara, ambayo ina jumla ya kemikeli zipatazo 7,000, unaweza kuharibu viungo vya ndani vya kijusi na unaweza kusababisha madhara ya kudumu.

Matokeo ya utafiti wa hivi karibuni uliofanyika kwa ushirikiano wa vyuo vikuu vya Aberdeen na Glasgow, pia ulibainisha athari tofauti za uvutaji wa sigara kwa vijusi vya kike na kiume.

Nyama za ini la kijusi cha kiume zilionekana kuwa na makovu huku muundo mzima wa seli za ini za kijusi cha kike zikionekana kuharibika.

Profesa Paul Fowler...mkurugenzi wa taasisi ya sayansi ya tiba katika chuo kikuu cha Aberdeen, amesema: "kazi hii ni sehemu ya mradi unaoendelea unaolenga kutambua namna uvutaji wa sigara kwa akina mama wajawazito unavyosababisha athari hatari katika ukuaji wa vijusi.

" Matokeo haya ya utafiti yanatoa mwanga zaidi juu ya tofauti za kimsingi katika uharibifu unaotokea baina ya vijjusi wa kike na wa kiume wakati mama mjamzito anapovuta sigara."