India: Msanii wa filamu India akosolewa kwa kumuonyesha miguu Narendra

Priyanka Chopra pamoja na Nahindra Modi Haki miliki ya picha Priyanka Chopra
Image caption Priyanka Chopra alituma picha hii kwenye Facebook

Mchezaji filamu mashuhuri wa India Priyanka Chopra amekosolewa na watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa kuamua kuvaa gauni linaloonyesha miguu yake alipokutana na waziri mkuu wa India Narendra Modi.

Baadhi ya watumiaji wa Facebook walimwambia kuwa "alimkosea heshma " waziri mkuu".

Haki miliki ya picha Avani Borkar
Image caption Walimkosoa kwa kutovalia vazi la kufunika miguu
Haki miliki ya picha Shirish Moreshwar Panwalkar
Image caption Walimwambia angepaswa kufunika miguu yake mbele ya waziri mkuu

Mchezaji filamu huyo ambaye hakuomba msamaha alijibu kauli hizo za ukosoaji kwa kutuma picha akiwa na mama yake wote wakiwa wamevalia gauni fupi, yenye maandishi "miguu ya siku".

Wachezaji filamu wengine wa India pia wamekuwa wakilengwa na hasira za wakosoaji wa mavazi wanayochagua kuyavaa.

Haki miliki ya picha PRIYANKA CHOPRA
Image caption Kujibu ukosoaji Priyanka Chopra alituma picha akiwa na mama yake wakiwa wamevalia nguo fupi

Deepika Padukone wakati mmoja alililaumu gazeti la India kwa kuchapisha picha iliyoonyesha matiti yake mnamo 2014.

"NDIO! Mimi ni mwanamke. Nina matiti ! unashida!!??" Padukone aliutuma ujumbe wa twitter kwa gazeti. Wachezaji filamu wengine pia walijitokeza kumtetea.

Priyanka Chopra: Sipendi kulipwa pesa kidogo kuliko wanaume.

'nachukia kwamba tunaitwa Bollywood'

Utata ulianza baada ya Chopra, aliyecheza katika filamu ya the new Baywatch na katika kipindi cha marekani cha Quantico, alipotuma picha akiwa na Bwana Modi, akimshukuru "kwa kukuchukua muda licha ya kuwa na ratiba ya shughuli nyingi" kukutana naye mjini Berlin.

Sikufikiria hata kabla hata hivyo kwamba gauni la "kukosa heshima " litakuwa mada ya mazungumzo, huku wengi wakitoa kauli zao juu ya namna lili "mtusi " Bwana Modi na "wafuasi wake sugu."