Trump akejeliwa baada ya kuandika neno lisilo na maana kwenye twitter yake

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Donald Trump aliandika neno kwenye Twitter lililokejeliwa na watumiaji wa internet

Neno moja la Bwana Trump limegubika mtandao wa internet leo Jumatano nalo ni: "covfefe".

Ni neno lililochapishwa kwenye wa mtandao twitter na rais wa Marekani Donald Trump, na watumiaji wa mtandao wa internet wamekuwa wakilitumia kumkejeli bila huruma.

" Licha ya kuendelea kwa ''covfefe'' za vyombo vya habari ,"alitwitt rais Trump baada ya saa sita usiku , kwa saa za Washington.

Halafu inavyoelekea baada ya ujumbe huo alikwenda kulala, bila kukamilisha wazo lake au kukosoa makosa yake ya kiuandishi.

Ilimchukua saa sita kabla ya kukubali makosa yake ndipo alipojibu kwa ucheshi , na wakati huo watu wengi walikuwa tayari wamekwishatuma jumbe za kejeli zao kwenye mitandao ya kijamii kuhusu neno ''covfefe''

Haki miliki ya picha Donald Trump Twitter
Image caption Baadhi walifanya kusudi kujaribu kutamka neno hilo, huku wakijiuliza mbona washirika wake hawakuweza kuingilia kati kumfahamisha kuhusu kosa alilolifanya

Ingawa ilionekana huenda neno alilonuwia kuandika lilikuwa ni "coverage", watumiaji wa mitandao ya kijamii ya habari walikuwa wakijaribu kubashiri kubashiri kile alichotaka kukiandika na lengo la kuandika neno hilo .

Baadhi walifanya kusudi kujaribu kutamka neno hilo, huku wakijiuliza mbona washirika wake hawakuweza kuingilia kati kumfahamisha kuhusu kosa alilolifanya.

Tafsri ya Google ililitambua neno hilo kama Samoan, ingawa haikutoa tafsiri yake kwa lugha ya kiingereza.

Msomaji mmoja wa taarifa za BBC rameandika akihoji ikiwa neno hilo linamaanisha kwamba rais Trump ni mzungumzaji wa kisiri wa lugha ya Samoa.