Bomu la kutegwa, laua 80 Kabul na kujeruhi kadhaa

Baadhi ya waathiriwa wa bomu hilo Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Baadhi ya waathiriwa wa bomu hilo

Watu 80 wameuawa na wengine zaidi ya mia tatu kujeruhiwa, baada ya bomu lililotegwa kwenye gari kulipuka mjini Kabul.

Maafisa nchini humo wanasema mlipuko mkubwa ambao umetokea katika eneo la makazi ya wanadiplomasia mapema asubuhi.

Wingu la moshi mkubwa lilikuwa limetanda na kuonekana katika maeneo mengi ya mji wa Kabul.

Aidha nyumba zilizokuwa jirani na bomu hilo lilipolipuka pia zilipatwa na madhara kwa madirisha na milango kupasuka.

Mwezi uliopita wapiganaji wa Taliban walitangaza kuanza kufanya mashambulizi na kusema kuwa yatakuwa yanalenga majeshi ya kigeni.