Wanajeshi wakichoma moto kituo cha polisi Nigeria

Kituo cha polisi kilichochomwa moto Nigeria Haki miliki ya picha Nigerian police
Image caption Kituo cha polisi kilichochomwa moto Nigeria

Ripoti kutoka nchini Nigeria zinasema Maafisa wa jeshi la Wanamaji wamevamia na kuchoma moto kituo cha polisi mjini Calabar kusini mwa nchi hiyo.

Maafisa wa polisi watatu wanaripotiwa kuuawa, ingawa bado haijafahamia vifo hivyo vimetokeaje.

Tukio hilo limetokea kufuatia mabishano yaliyotokea katika wanajeshi hao wa majini na maafisa wa polisi.

Ripoti zaidi zinasema maafisa hao wa jeshi la maji walirudi tena katika eneo hilo wakiwa wamejiimarisha zaidi na kuanza kushambulia kituo cha polisi, na baadaye kukichoma moto.