Upinzani Tanzania wapata pigo

Philemon Ndesamburo Haki miliki ya picha Tanzania Media
Image caption Philemon Ndesamburo

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimepata pigo kubwa baada ya kuondokewa na mmoja wa waasisi wake.

Akithibitisha taarifa hizo, msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene, amesema Philemon Kiwelu Ndesamburo aliyezaliwa mwaka 1935 amefariki leo, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Marehemu ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Moshi kwa kipindi kirefu, kupitia CHADEMA, ndiye mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo, mpaka hii leo mauti yalipomkuta.

Atakumbukwa zaidi kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwa chama hicho cha upinzani, hususan katika kukifadhili chama kwa hali na mali.