Trump kutangaza msimamo wake kuhusu makubaliano ya Paris

Paris
Image caption Makubaliano ya Paris juu ya kukabiliana na hewa chafu

Vyombo vya habari vya marekani vinasema rais Trump anatarajia kutangaza kujitoa kwenye makubaliano ya mabadiliko ya tabia nchi yaliyowekwa mjini Paris,Ufaransa.

Rais Trump mwenyewe aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa anatoa tangazo hilo hivi karibuni.

Image caption Makubaliano ya mabadiliko ya tabia nchi,Paris

Kujitoa katika harakati hizo za mabadiliko ya tabia nchi ni miongoni mwa vipaumbele ambavyo alivitaja wakati wa kampeni zake za urais ingawa hivi karibuni rais huyo alikaririwa kusema kuwa bado hajafanya maamuzi.

Mkutano wa nchi zenye uchumi mkubwa G7 uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ,uliolenga kupunguza shughuli zinazongeza uzalishaji wa hewa chafu ili kupuguza athari za mabadiliko ya tabia nchi kama ilivyokubaliana na nchi takribani mia mbili jambo ambalo rais Trump alikuwa hajaliridhia.

Mada zinazohusiana