Kampuni yakiri kutoa dola bilioni 3 kama rushwa Brazil

Rais Temer amesema kashfa hiyo imetengenezwa na wanasiasa wasiompenda
Image caption Rais Temer amesema kashfa hiyo imetengenezwa na wanasiasa wasiompenda

Kampuni kubwa duniani ya kusindika nyama iliyopo nchini Brazil, imekubali kwamba iliilipa serikali ya nchi hiyo kiasi cha zaidi ya dola Bilioni tatu katika kile kinachotajwa kuwa ni rushwa kubwa zaidi nchini humo.

Waendesha mashitaka nchini humo wanasema kuwa faini hiyo ilikuwa kubwa kupitiliza.

Image caption Waandamanaji wanataka Rais Temer kuachia madaraka kwa kashfa hiyo

Mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo Joesley Batista anatuhumiwa kupanga njama na Rais Temer ili kupoteza ushahidi.

Rais Temer amesema kamwe hatoachia madakara kwa kashfa hiyo ambayo anadai ni ya kutengenezwa.