Idadi ya mapacha wanaokufa barani Afrika ni ya kutisha

Watoto mapacha Haki miliki ya picha SCIENCE PHOTO LIBRARY
Image caption utafiti unasema kuwa mafanikio katika kunusuru maisha ya mapacha yamekuwa nyuma ya yale ya kunusuru maisha ya watoto wengine

Mtoto mmoja kati ya watano wanaozaliwa mapacha katika eneo la kusini mwa jangwa la sahara barani Afrika hufa kabla ya kutimiza umri wa miaka mitano, kulingana na utafiri mpya uliochapishwa katika jarida la Lancet.

Utafiti huo ni wa kwanza wa kuchunguza viwango vya vifo miongoni mwa watoto mapacha kusini mwa jangwa la sahara barani Afrika.

Ripoti hiyo inasema kuwa mafanikio katika kunusuru maisha ya mapacha yamekuwa nyuma ya yale ya kunusuru maisha ya watoto wengine.

Viwango vya vifo miongoni mwa watoto wanaozaliwa akiwa mmoja wenye umri wa chini ya miaka mitano ilipungua kwa nusu baina ya mwaka 1995 na 2014.

Kwa mapacha, viwango vyao vilipungua kwa theluthi.

Kujifungua watoto mapacha ni hatari zaidi ya kujifungua mtoto mmoja - bila kujali ni nchi gani mama aliyojifungulia.

Hatari huongezeka kwa wale wanaojifungua mapema, kujifungua watoto wenye uzito mdogo na wakina mama kupoteza damu nyingi.

Lakini utafiti unasema kuwa hatari hizi "hunajumuinsha " kwa viwango vya hali ya juu, huduma duni za uzazi na huduma kwa watoto wachanga miongoni mwa nchi zilizoko kusini mwa jangwa la sahara barani Afrika.

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Kujifungua watoto mapacha ni hatari zaidi ya kujifungua mtoto mmoja - bila kujali ni nchi gani mama aliyojifungulia.

Katika nchi ya Finland ambayo kwa mfano ina huduma bora za uzazi duniani - watafiti wanasema kwa kila mapacha 1,000 wanaozaliwa, 11 kati yao hufa kabla ya kutimiza umri wa mwaka mmoja.

Kulingana na utafiti kati ya mapacha 1000 wanaozaliwa 137 hufa kabla ya kuadhimisha mwaka mmoja wa kuzaliwa.

Na mapacha 213 kati ya 1,000 hufa kabla ya kutimiza umri wa miaka mitano.