Nyota wa NBA LeBron James asema ubaguzi wa rangi Marekani hautaisha

LeBron James Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maafisa husika wanatathmini picha za uchunguzi ili kubaini muhusika aliyechora mchoro huo wa kumtusi mtu mweusi kwnye nyumba ya LeBron James

Nyota wa mchezo wa kikapu katika NBA LeBron James amezungumzia kuhusu masaibu ya muda mrefu ya ubaguzi baada ya "Neno-N" la kumtusi mtu mweusi lilipochorwa kwenye nyumba yake ya Los Angeles.

"Hata uwe na pesa kiasi gani , hata uwe na umaarufu kiasi gani ... Kuwa mtu mweusi nchini Marekani ni vigumu ," alisema.

Mchoro huouliripotiwa na polisi Jumatano asubuhi na nyota huyo wa timu ya Cleveland Cavaliers alijibu saa kadhaa baadae.

Maafisa wa LAPD waliithibitishia BBC juu ya kuwepo kwa mamakosa mashtaka makubwa ya ubaguzi wa rangi.

Maafisa husika wanatathmini picha za uchunguzi ili kubaini muhusika aliyechora mchoro huo.

James alikuwa akizungumza kutoka San Francisco, ambako timu yake imepiga kambi ya mazoezi kabla mchezo wa 1 wa fainali za NBA.

"Ubaguzi wa rangi siku zote utakuwa sehemu ya dunia, sehemu ya Marekani, na chuki nchini Marekani - hasa kwa waMarekani wenye asili ya Afrika - upo kila siku ," alisema .

Aliongeza kusema kuwa : "tuna safari ndefu sisi kama jamii na sisi kama waMarekani wenye asili ya Afrika hadi tutakapohisi tuko na usawa Marekani."

LeBron James mwenye umri wa miaka 32 anatambuliwa kama mchezaji wa anayelipwa zaidi katika NBA, akiripotiwa kulipwa kitita cha zaidi ya dola milioni 30 ($30m) kwa mwaka.

Wiki iliyopitaaliytangazwa kama mchezaji aliyefunga vikapu vingi zaidi katika mchezo wa kikapu nchini Marekani , akivunja rekodi ya nyota wa zamani wa Chicago Bulls Michael Jordan.