Polisi wawili wauawa na wauzaji wa mihadarati Peru

Jimbo la Apurimac-Ene ni maarufu kwa biashara za madawa ya kulevya
Image caption Jimbo la Apurimac-Ene ni maarufu kwa biashara za madawa ya kulevya

Askari polisi wawili wamepigwa risasi na kuuawa nchini Peru na watu wanaodhaniwa kuwa ni wauzaji wa dawa za kulevya.

Walishambuliwa walipokuwa wakitoka katika doria kwenye mji wa Apurimac-Ene, mji ambao ni maarufu kwa ukuuzaji wa dawa za kulevya.

Rais wa nchi hiyo Pedro Pablo Kuczynski wamefanya tukio hilo ikiwa ni kulipiza kisasi cha kuharibiwa kwa zaidi ya kilo 700 za dawa za kulevya.

Biashara ya dawa za kulevya katika jimbo hilo inaendeshwa na kundi la waasi la Shining Path.