China inataka kuwa nchi ya mfano katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

China
Image caption Mabadiliko ya tabia nchi

China imeahidi kutekeleza majukumu yake katika makubaliano yaliyowekwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi licha ya kuwa Marekani haitoshiriki katika makubaliano hayo.

Akizungumza nchini Ujerumani waziri mkuu wa China, Li Keqiang amesema inapenda kukabiliana na suala la mabadiliko ya tabia nchi.

Na kuongeza kuwa, nchi yake, inataka kuwa nchi ya kupigiwa mfano katika harakati za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa upande wake, rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kutangaza maamuzi yake kuhusiana na makubaliano ya Paris ya mwaka 2015 hapo baadae, huku baadhi ya taarifa kutoka nchini Marekani

zinasema kuwa rais Trump atajiondoa katika mkataba huo.

Image caption Waziri Li Keqiang

"China itaendea kutekeleza makubaliano yaliyofanywa katika mkutano wa Paris lakini pia tunatarajia kuyafanya haya kwa kushirikiana na nchi nyingine," alisema waziri Li.

China ikiwa miongoni mwa mataifa makubwa ambayo imeamua kutekeleza majukumu yake katika kujaribu kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Image caption Li Keqiang amesema inapenda kukabiliana na suala la mabadiliko ya tabia nchi.

Urusi pia imesema itaendelea kubaki katika wajibu wake kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa lakini wamesema kuwa makubaliano hayo yatapata pigo iwapo Marekani itajitoa.

"Tunaendelea bila kusema kwamba ufanisi wa mazungumzo haya utakuwa umepoteza nguvu kwa kukosekana kwa washiriki wake wakuu," amesema Kremlin.

Kwa sasa waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Boris Johnson amesema alikuwa na shauku kuhusiana na uamuzi wa Marekani kujiondoa na kuongeza kwamba anaamini rais Trump angelitafakari suala hilo kwa namna ya pekee.

Mada zinazohusiana