Ethiopia yazima mawasiliano ya huduma za intaneti

Ethiopia
Image caption Ethiopia yazima mawasiliano ya huduma za intaneti

Serikali ya Ethiopia imezima mawasiliano yote ya huduma za mtandao wa Intaneti kwenye simu za mkononi kuzuia uvujaji wa mitihani kwenye mitandao.

Mnamo mwaka jana, nchi hiyo iliripotiwa kubana mawasiliano ya mitandao ya kijamii mara baada ya mitihani ya chuo kikuu kuvuja kwenye mitandao.

Afisa habari wa taasisi ya mawasiliano nchini humo ,Mohammed Seid amesema hatua hiyo ya kuifungia mitandao inatokana na sababu ileile ya mwaka jana ili kuzuia wanafunzi wasiibe mitihani.

Hali ya hatari iliyopo nchini Ethiopia tangu mwezi Oktoba mwaka jana imesababisha maamuzi hayo kufanyika.

Huduma ya intaneti kupitia simu za mkononi imekuwa ikifungwa mara kwa mara nchini humo.