Wahamiaji zaidi ya 40 wamekufa kutokana na kiu katika Jangwa la Sahara

Image caption Wahamiaji zaidi ya 40 wamekufa kutokana na kiu baada ya gari lao kuharibika katika Jangwa la Sahara kaskazini mwa Niger

Wahamiaji zaidi ya 40 wamekufa kutokana na kiu baada ya gari lao kuharibika katika Jangwa la Sahara kaskazini mwa Niger.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu limeseama kuwa watu sita waliosalimika ni wanawake ambao walipata msaada baada ya kutembea katika kijiji cha mbali.

Taarifa zinasema, miongoni mwa waliokufa ni pamoja na watoto.

Vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti kuwa miongoni mwa wahamiaji hao wametoka nchini Ghana na Nigeria ambapo walikuwa wanajaribu kuingia Libya.

Licha ya kuwa hamna muwakilishi kutoka taifa lolote baina ya hayo mawili amabae amefika katika eneo hilo.

Image caption Wahamiaji wamekufa kutokana na kiu

Njia inayotoka Niger kuelekea Libya ni miongoni mwa njia kuu ambayo watu kutoka Afrika Magharibi huitumia kuvuka bahari ya Mediterania ili kuingia Bara la Ulaya.

Mada zinazohusiana