Vifo vitokanavyo na magonjwa ya kuhara vimepungua kwa watoto

Maji machafu ni chanzo kimojawapo cha magonjwa ya kuhara
Image caption Maji machafu ni chanzo kimojawapo cha magonjwa ya kuhara

Utafiti mpya umeonyesha kuwa idadi ya watoto wanaofariki duniani kwa ugonjwa wa kuhara imepungua kwa robo tatu tokea mwaka 2005 mpaka 2015.

Katika jarida la afya la The Lancet, watafiti kutoka nchini Marekani wamesema mafanikio hayo yamesababishwa na upatikanaji wa maji safi na salama sambamba na mazingira bora.

Lakini taarifa hiyo inasema kuwa ugonjwa wa kuhara ni wa nne kwa kuua watoto wengi duniani kote, ikiwa ni sawa na nusu milioni kila mwaka na hii ni kwa umri chini ya miaka mitano.

Vifo vingi hutokea nchi za Nigeria na India.