Ujerumani haitawafukuza raia wa Afghanistan

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel pia alilaani tukio la shambilizi la Kabul
Image caption Kansela wa Ujerumani Angela Merkel pia alilaani tukio la shambilizi la Kabul

Ujerumani imesitisha kuwafukuza raia wa Afghanistan wengi nchini humo ambao maombi yao ya kuhifadhiwa yalikataliwa, kutokana na mlipuko mkubwa wa bomu siku ya Jumatano huko Kabul.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani inasema mbinu mpya za kiusalama zitafanyika mwezi Julai katika ubalozi wake wa Kabul ambao uliharibiwa vibaya katika mlipuko huo.

Imesema pia itawafukuza wote wanaohusishwa na matukio ya kigaidi, pamoja na wale wanaotafuta hifadhi ambao hukataa kujitambulisha.

Ujerumani inaendelea kuwasaidia walioomba hifadhi kutokea Afghanistan ambao wako tayari kurejeshwa makwao kwa hiari.

Watu 90 waliuawa na wengine 400 walijeruhiwa katika shambulizi hilo la Kabul.

Mada zinazohusiana