Gari lalipuka Mashariki mwa Saudi Arabia

Hakukuwa na majeruhi katika gari hilo
Image caption Hakukuwa na majeruhi katika gari hilo

Gari moja limelipuka Mashariki mwa Saudi Arabia katika mji wa Qatif ambapo video ya mlipuko inaonyesha ilivyokuwa inaungua moto katikati ya barabara.

Picha nyingine zinaonyesha mwili uliounguzwa ukiwa umelala kando gari.

vyanzo vya habari nchini humo vinasema kwamba watu wawili waliokuwemo katika gari hilo walifariki.

Polisi wanasema kuwa baada ya ukaguzi walikuta gari hilo likiwa na risasi pamoja na mabomu.

Pamekuwepo na machafuko pamoja vurugu za hapa na pale pale kwa miaka ya hivi karibuni kwenye mji huo huku wanaharakati wa Shia na waandamanaji walipambana na vikosi vya usalama.