Watoto na hamu ya kusoma vitabu

Mtoto akijisomea Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mtoto akijisomea

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya taifa ya Kujua kusoma na Kuandika nchini Uingereza umeonesha kuwa theluthi moja ya wavulana nchini humo wanasema wanafurahia kusoma vitabu.

Taasisi hiyo imegundua kushuka kupenda kusoma vitabu kwa wavulana kati ya umri wa miaka minane mpaka 16.

Asilimia 72 ya wavulana wenye umri kati ya miaka minane mpaka 11, waliohojiwa walionesha kupenda kusoma, lakini asilimia hiyo imeshuka mpaka kufikia asilimia 36 wanapofika umri wa miaka 14 mpaka 16.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mambo mengi yanachangia kushuka kwa mapenzi ya kusoma vitabu kwa vijana

Aidha mapenzi ya wasichana pia katika kusoma vitabu inashuka pia kadri umri unavyoongezeka.

Wasichana waliohojiwa kati ya umri wa miaka minane mpaka 11, asilimia 83 walikuwa wakifurahia kusoma vitabu, lakini asilimia hiyo ilishuka mpaka 53 kwa wasichana wa umri wa miaka 14 mpaka 16.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo Jonathan Douglas mapenzi ya vijana kupenda kusoma vitabu yamekuwa yakipungua kwa kasi baada ya kumaliza shule.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wazazi na Walimu wanatakiwa kuwahamasisha vijana kupenda kusoma vitabu

Hata hivyo amesema kuna njia nyingi ambazo wazazi na walimu wanaweza kuzitumia kuwahamasisha vijana hawa kupenda kusoma vitabu.

Ametolea mfano vitabu vya michezo kama vile mpira wa miguu, ucheshi magazeti na pia kuwaachia wenyewe wachague wanachpenda kusoma.