Ghasia zaendelea Morocco

Mwanaharakati Nasser Zefsafi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanaharakati Nasser Zefsafi

Mgomo mkubwa unaofanyika katika mkoa ulio kaskazini mwa Morocco umeingia siku ya pili leo kama sehemu ya maandamano kutaka kuachiwa kwa kiongozi wa upinzani nchini humo.Mgomo mkubwa unaofanyika katika mkoa ulio kaskazini mwa Morocco umeingia siku ya pili leo kama sehemu ya maandamano kutaka kuachiwa kwa kiongozi wa upinzani nchini humo.

Maandamano hayo yanafuatia kukamatwa kwa Nasser Zefsafi ambaye ni mwanzilishi wa harakati zinazotaka kuwepo kwa vitega uchumi zaidi na ajira katika eneo lao.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandamanaji

Waandamanaji walifunga mitaa baada ya mwanaharakati huyo kukamatwa Jumatatu kwa makosa ya kuhujumu usalama wa taifa.

Zefsafi anadaiwa kupanga maandamano dhidi ya rushwa na ukosefu wa ajira.

Morocco inadaiwa kukumbwa na ghasia za maandamano tangu kutokea kifo cha mchuuzi wa samaki Al- Hoceima Oktoba mwaka jana.

Maandamano pia yanaelezwa kufanyika katika mji wa Casablanca na pia mji mkuu Rabat.