Msichana wa miaka 20 amepata ufuasi mkubwa wa Facebook kwa kuigiza nyimbo za Beyoncé

Msichana wa miaka 20 amepata ufuasi mkubwa wa Facebook kwa kuigiza nyimbo za Beyoncé

Msichana mwenye umri wa miaka ishirini ameweza kupata kura za watu zaidi ya milioni moja katika Facebook , kutokana na kuigiza nyimbo za mwana muziki wa marekani Beyoncé.

Wapenzi wa msichana huyo Iteriteka Christa Verra Audrey tayari wamembatiza Beyoncé wa Burundi.

Huyu ni mwanafunzi wa darasa la 12 la sekondari katika shule moja wapo katikati mwa Burundi.Video yake akiimba baadhi ya nyimbo za Beyoncé, imezunguka dunia nzima tokea mwaka 2015.

Mwandishi wetu Ismail Misigaro amepata fursa ya kuzungumza nae na kutuandalia taarifa ifuatayo.