Kijiji kilichobaki mahame kutokana na mauaji Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Kijiji kilichobaki mahame kutokana na mauaji Tanzania

Viongozi katika wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani nchini Tanzania ambako kumetokea mfululizo wa vitendo vya mauaji, wanasema hawaamini kama chanzo cha mauaji hayo ni matokeo ya kile ambacho kinadaiwa kuwa ni dhuluma na unyanyasaji wa viongozi wa vijiji hivyo.

Hadi sasa zaidi ya viongozi 30 wameuwawa huku ikiwa hakuna aliyekamatwa kuhusishwa na mauaji hayo.

Lakini wakati serikali ikiendelea na uchunguzi.

mwandishi wetu Sammy Awami alitembelea kijiji cha Nyambunda, moja kati ya vijiji vilivyoathirika na mauaji hayo, na kutuandalia taarifa ifuatayo.

Mada zinazohusiana