Al Shabab wavamia Kambi ya jeshi la Kenya Kolbiyow

Hii si mara ya kwanza al shabab wanavamia kambi za jeshi la Kenya Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Hii si mara ya kwanza al shabab wanavamia kambi za jeshi la Kenya

Ripoti kutoka kusini mwa somali zinazema kambi ya wanajeshi wa Kenya imevamiwa viungani mwa mji wa Kulbiyow nchini Somalia.

Milipuko kadhaa iliripotiwa kusikika kutoka eneo hilo.

Inaarifiwa kuwa vikosi vya Kenya vimejibu vikali uvamizi huo.

Mapema mwaka huu, maafisa kadhaa wa Kenya waliuwawa na wanamgambo wa Al shabaab waliovamia kambi yao.

Image caption Somalia