Ireland kupata waziri mkuu wa kwanza mpenzi wa jinsia moja

Leo Varadkar Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Leo Varadkar 38 atakuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi Ireland

Leo Varadkar anatarajiwa kuwa waziri mkuu nchini Ireland baada ya kushinda uongozi kwa chama cha Fine Gael.

Varadkar mwenye umri wa miaka 38, atakuwa waziri mkuu wa kwanza mpenzi wa jinsia moja na pia waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi kuwaia kuongoza nchi hiyo.

Bwana Varadkar alimshinbda wazari wa makao Simon Ceveney kwa asilimia 60 ya kura kuongoza chama cha Fine Gael, ambacho ndicho chama kikubwa zaidi katika serikali ya umoja.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Leo Varadkar akiwapungia mkono wafuasi

Atachukua mahala pa Enda Kenny kama kiongozi wa chama cha kati kulia wiki chache zinazokuja.

Alijulikana kuwa mpenzi wa jinsia moja wakati wa kura ya maoni ya ndoa za jinsia moja mwaka 2015.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Leo Varadkar akipongezwa na Simon Coveney