Aliyewaua watoto Canada azuiwa kutoa huduma shuleni

Karla Homolka Haki miliki ya picha Canadian Press
Image caption Karla Homolka mwaka 1993

Mmoja wa watu waliojulikana kwa kuwaua watoto nchini Canada amefahamishwa kuwa kamwe hawezi kufanya kazi ya kujitolea katika shule mmoja ya msingi, kufuatia kilio kutoka kwa umma.

Karla Homolka alitumikia kifungo cha miaka 12 jela kutokana na makosa ya ubakaji na mauaji ua wasichana wawili wa shule katika kisa ambacho kiliitamausha nchi.

Iliibuka wiki hii kuwa alikuwa akisaidia katika shule ya watoto wake ya kibinafsi iliyo Monreal.

Homolka mwenye umri wa miaka 47, aliachiliwa kutoka gereza lenye ulinzi mkali huko Quebec mwaka 2005.

Shule aliyokuwa akihudumu ilipokea malalamishi mengi kutoka kwa wazazi na umma.

Homolka na mumewe wa zamani Paul Bernado waliwaua wasichana wa shule huko Ontario mapema miaka ya 90.

Homolka pia alishiriki katika ubakaji na mauaji ya mwaka 1990 na dadake wa umri wa miaka 15.

Lakini alipewa kifungo chepesi mwaka 1993 baada ya kukubali kutoa ushahidi dhidi ya Bernado.

Bernado alipewa kifungo cha maisha na bado yuko gerezani huko Ontario.