Aliyekuwa mke wa Charles Taylor kujibu mashtaka Uingereza

Agnes Taylor pictured in the early 1990s
Image caption Agnes Reeves Taylor miaka ya 190 - alikamatwa siku ya Alhamisi

Aliyekuwa mke wa wa rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor amefikishwa katika mahakama ya Westminister mjini London kujibu mashtaka ya mateso.

Agnes Reeves Taylor mwenye umri wa miaka 51 anashukiwa kuamuri kufanywa mateso kati ya mwaka 1989 na mwaka 1991 wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Hadi watu 250,000 wanaamika kuuliwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia vilivyomalizika mwaka 2003.

Bi Reeves Taylor alikamatwa siku ya Alhamisi. Hajazungumzia lolote kufuatia kukamatwa kwake.

Mashtaka mengine yanasema kuwa yeye na watu wengine ambao hawajuliaani walimtesa katika yaliyakuwa makao ya Taylor ya Gbarnga.

Taylor alihudumu kama rais kutoka mwaka 1997 hadi mwaka 2003 wakati alilazimishwa kukimbilia uhamishoni.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Charles Taylor(kushoto)

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii