Aliyetetea ukoloni afukuzwa chamani Afrika Kusini

Helen Zille ni mwanasiasa maarufu Afrika Kusini Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Helen Zille ni mwanasiasa maarufu Afrika Kusini

Chama kikuu cha upinzani cha Afrika Kusini, Democratic Alliance, kimesimamisha uanachama wa kiongozi wake wa zamani, Helen Zille, kwa sababu ya tweet aliyoandika, ambapo alisema, siyo ukoloni wote mbaya.

Kiongozi wa sasa wa chama, Mmusi Maimane, alisema hata hivyo, Bibi Zille atabaki na wadhifa wake, kuwa waziri kiongozi wa Jimbo la Cape Magharibi.

Chama cha Democratic Alliance kimeshinikizwa Bibi Zille achukuliwe hatua tangu tweet zake kuzusha utatanishi awali mwaka huu.

Mwandishi wa BBC anasema, chama cha Democratic Allience, kinajaribu sana kuondosha wazi, kwamba kwa jumla, kinawakilisha masilahi ya wazungu wa Afrika Kusini.

Haki miliki ya picha Twitter - @helenzille
Haki miliki ya picha Twitter - @helenzhille