Mshambuliaji wa Casino Ufilipino atambuliwa na polisi

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Idara ya Polisi ilitoa picha hii ya mshambuliaji mara baada ya shambulio hilo

Vyombo vya usalama nchini Ufilipino, vinasema kuwa vimemtambua mshambuliaji ambaye aliwauwa watu 30 katika eneo moja la kuchezea mchezo wa kamari katika mji mkuu Manila, Ijumaa iliyopita.

Wakuu hao wanasema kuwa alikuwa mfilipino kwa jina Jessie Javier Carlos, ambaye ana madeni makubwa ya uchezaji kamari na hakuwa gaidi.

Afisa mkuu wa polisi mjini Manila, Bwana Oscar Al-bayalde, amewaambia waandishi habari kuwa, wanaamini shambulio hilo lilitekelezwa na mtu mmoja tu.

Mtu huyo aliyekuwa amefunika uso wake, aliingia katika eneo la kuchezea- kamari liitwalo Resorts World Casino na kuanza kuwamiminia watu risasi, kabla ya kuteketeza ukumbi wa kuchezea kamari.

Alipatikana akiwa amefariki saa chache baadaye.