Tamasha la mjini Manchester lafana

Uingereza

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha,

Tamasha la One Love mjini Manchester ,mwanamuziki Ariana Grande akitumbuiza

Mwanamuziki maarufu nchini Marekani Ariana Grande , ambaye tamasha lake lilikumbwa na mushkeli mjini Manchester baada ya mtu mmoja kujitoa muhanga wiki mbili zilizopita, amekwea tena jukwaani katika mji huo wa waingereza, kufanya tamasha kubwa kwa heshima ya waathirka wa shambulio hilo.

Katika shambulizi hilo la wiki mbili zilizopita la kujioa muhanga watu ishirini na wawili walipoteza maisha .Wasanii wakubwa katika tasnia ya muziki walihudhuria katika tamasha hilo lililopewa jina One Love Manchester benefit concert, wasanii akiwemo Coldplay na Justin Bieber walitumbuiza .

Wasanii walisikika wakiwaambia watu wapatao elfu hamsini waliohudhuria tamasha hilo kwamba chuki na woga havitakuwa na nafasi ya kujitwalia ushindi, wakati hayo yakijiri, kulikuwa na ulinzi mkali wakati wa tamasha hilo la heshima.

Taarifa kutoka mjini Manchester zinaarifu kuwa zaidi ya tiketi elfu kumi na nne zitaelekezwa kwa watu waliohudhuria katika tamasha lililopita na kushambuliwa.