Putin akana uhusiano na aliyekuwa mshauri wa Trump Michael Flynn

Michael Flynn (wa pili kushoto) na Rais Vladimir Putin (wa pili kulia) waliketi pamoja mjini Moscow mwaka 2015

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Michael Flynn (wa pili kushoto) na Rais Vladimir Putin (wa pili kulia) waliketi pamoja mjini Moscow mwaka 2015

Rais wa Urusi Vradimir Putin ameliambia shirika la utangazaji la Marekani NBC kwamba alizungumza kwa nadra sana na mshauri wa zamani wa masuala ya usalama wa Marekani , Michael Flynn.

Wawili hao walikuwa wameketi pamoja kwa chakula cha jioni mjini Moscow miezi kumi na tisa iliyopita.

Picha iliyosambazwa ya tukio hilo ilichochea uvumi juu ya uhusiano baina ya utawala wa Trump na Moscow.

Bwana Putin alikimbia kituo cha Marekani NBC kuwa alikuja kujulishwa baadaye kuwa Flynn alikuwa ni nani.

Bwana Flynn alifutwa mwezi Februari baada ya kuidanganya Ikulu ya White House kuhusu uhusiano wake na Urusi.

Baadaye Bwana Flynn alikataa kufika mbele ya kamati ya bunge kuelezea uhusiano wake na Urusi na madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa mwaka 2016 nchini Marekani.