Ajali ya basi yaua watu 22 India

Map of Bareilly
Maelezo ya picha,

Bareilly India

Takriban watu 22 wameuwawa baada ya basi walimokuwa wakisafiria kugongana na lori kwenye mkoa ulio kaskazini mwa India wa Uttar Pradesh.

Ajali hiyo ilitokea mapema leo Jumatatu katika mji wa Bareilly kilomita 252 kutoka mji mkuu wa jimbo Lucknow.

Afisa wa cheo cha juu cha polisi alisema waathiriwa wote kwenye ajali hiyo walikuwa na majeraha mabaya na hawatambuliwa mara moja.

Basi hilo la abiria lilishika moto kufuatia mgongano huo. Polisi wanamtafuea dereva wa lori lililohusika kwenye ajali.

Shirika la habari la AFP liliwanukuu polisi wakisema kuwa milango ya basi ilikwama baada ya mlipuko hali iliyosababisha abiria kukwama ndani ya basi.

Watu wachachee walifanakiw kutoka nje kwa kuvunja madirisha ya basi.

India ina viwango vya ju zaidi vya ajali za barabarani duniani ambapo ajali hutokea baada ya kila dakika nne.