Mabaki ya mwanamume yapatikana miaka 10 tangu atoweke Australia

Polisi walipata mabaki ya Bwana Matthew Leveson kichakani

Chanzo cha picha, ABC

Maelezo ya picha,

Polisi walipata mabaki ya Bwana Matthew Leveson kichakani

Mabaki ya binadamu yamepatiakana katika kichaka kikubwa nchini Australia ya mwanamume ambaye alitoweka miaka 10 iliyopita.

Matthew Leveson, ambaye alikuwa na umri wa miaka 20, alionekana mara ya mwisho akiondoka katika klabu moja mjini Sydney mwaka 2007, akiwa na rafiki yake Michael Atkins.

Bwana Atkins aliondolewa mashtaka ya mauaji ya bwana Leveson mwaka 2009.

Baadaye alipata makubaliano ya kuzuia kufunguliwa mashtaka ikiwa angetoa habari za ulipo mwili wa Leveson.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Polisi waiktafuta mabaki

Polisi walipata mabaki hayo katika bustani ya Sydney siku ya Jumatano. Uchunguzi wa DNA ulibainisha kuwa mabaki hayo yalikuwa ni ya bwana Leveson.

Wazazi wake, Faye na Mark Leveson waliweka maua eneo hilo wiki iliyopita.

"Tumepigana kwa muda wa maika tisa unusu hadi kufika siku hii na kumleta mtoto wetu nyumbani," Bwana Leveson aliwaambia waandishi wa habari.