Ajifungua mtoto ndani ya treni baada ya kukataliwa hospitalini Afrika Kusini

Wakati treni iliwasili mjini Johanneburg alikuwa amepata maumivi ya kujifungua kwa muda saa tano

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wakati treni iliwasili mjini Johanneburg alikuwa amepata maumivi ya kujifungua kwa muda saa tano

Mwanamke mmoja amejifungua mtoto akiwa ndani ya treni baada ya hospitali mbili kukataa kumlaza.

Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa IOL ni kuwa Francine Ngalula Kalala, alifukuzwa kutoka hospitali hizo kwa kuwayenye ni mtafuta hifadhi nchini humo.

Mtandao huo unasema kuwa alinyimwa matibaua kwenye hospitali mbili mjini Pretoria, ndipo akaingia ndani ya treni kuelekea mji mkuu wa Johannesburg.

Alikaa muda wa dakika 45 ndani ya treni akitabika huku abirai wengine wakijaribu kumsadia.

Wakati treni iliwasili mjini Johanneburg alikuwa amepata maumivi ya kujifungua kwa muda saa tano ndipo akajifungua eneo la kutembea abiria katika kituo cha treni.

Gari la wagonjwa likampeleka hospitalini na mtoto wake ambapo pia alinyimwa matibabu.

Hata hivyo hopitali ya nne ilikubali kumlaza na mtoto wake msichana.