Mti mrefu zaidi Afrika kivutio kipya cha watalii Tanzania

Mti mrefu zaidi Afrika kivutio kipya cha watalii Tanzania

Mkoa wa Kilimanjaro uliopo kaskazini mwa Tanzania, ni maarufu kwa shughuli za utalii.

Kila mwaka watalii huja kwa lengo la kupanda Mlima Kilimanjaro.

Lakini hivi sasa, watalii wamepata kivutio kingine mkoani humo. Hii ni baada ya serikali ya Tanzania kutangaza kuwepo kwa mti mrefu zaidi barani Afrika.