Khan: Sitamruhusu Trump kugawanya jamii

London
Image caption Meya wa mji wa London Sadiq Khan

Meya wa mji wa London, Sadiq Khan, amesema kwamba hatomruhusu Donald Trump kuzigawa jamii kufuatia shambulizi la mwishoni mwa juma lilopita, baada ya rais wa Marekani kumkosoa vikali kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Trump amemshutumu Meya huyo kwa kutoa sababu za uongo kwa kuwaambia watu wa London kwamba hakukuwa na sababu ya kuwa na wasiwasi.

Kwahakika yeye amesema kwamba watu hawakupaswa kuwa na wasiwasi baada ya kupelekwa askari wenye silaha mitaani.

Sadiq Khan ameiambia BBC kuwa baadhi ya watu walionekana kuchochea mgawanyiko. Msemaji wa Ikulu ya Marekani, alikanusha rais kujipatia sifa kupitia jina la meya huyo ambaye ni muislam wa kwanza kushika wadhifa huo.