EU kusaidia kupambana na ugaidi

Ufaransa Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Ufaransa Emanuel Macro alipovitembelea vikosi vya Ufaransa vilivyoko nchini Mali

Umoja wa Ulaya umekubali kutoa zaidi ya dola milioni hamsini kwa Muungano mpya wa pamoja barani Afrika wa nguvu za kijeshi katika ukanda wa eneo la ukanda wa jangwa la Sahara.

Majeshi hayo yataundwa katika vikundi vidogo vidogo kutoka katika nchi ya Mali, Mauritania, Chad, Burkina Faso na Niger, kwa lengo la kupamabana na wanamgambo wenye itikadi kali za kidini.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Mali , Abdoulaye Diop ametangaza kuwa jeshi hilo litajumuisha wanajeshi elfu kumi na polisi, ongezeko la mipango ya awali kwa askari elfu tano .

Na taarifa za awali zinaeleza kwamba utekelezaji wa mpango huo utakamilika mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu.