Mchezaji wa zamani wa Newcastle Cheick Tiote afariki akiwa mazoezini Uchina

Cheick Tiote Haki miliki ya picha PA
Image caption Mchezaji wa zamani wa Newcastle Cheick Tiote afariki akiwa mazoezini Uchina

Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Newcastle Cheik Tiote amefariki akiwa na umri wa miaka 30 baada ya kuzirai akiwa mazoezini nchini China

Katika kipindi cha miaka saba akiichezea United, mchezaji huo raia wa Ivory Coast alicheza mechi 150 zikiwemo mechi tatu katika msimu wake wa mwisho.

Alijiunga na ligi ya pili ya Uchina ya Beijing Enterprises akitokea Newcastle mwezi Februari.

Mzaliwa huyo wa Ivory Coast alikuwa katika kikosi cha Ivory Cosat kilichoshinda kombe la taifa bingwa barani Afrika mwaka 2015.

A;ainza kusakata soka ya kimataifa nchini Ubelgiji akiwa na klabu ya Anderlecht mwaka 2005, kabla ya kuhamia klabu ta ya FC Twente ya Uholanzi amabapo alishiriki mechi 86 na kushinda Ligi ya Eredivisie msimu wa 2009 na 2010 chini ya meneja Steve McClaren.

Kisha baadaye Tiote akajiunga na Newcastle mwaka 2010 kwa kitita cha pauni milioni 3.5.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tiote akajiunga na Newcastle mwaka 2010 kwa kitita cha pauni milioni 3.5.

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea