Polisi wachunguza kisa cha "ugaidi" Australia

Police from the bomb squad unit walk near scene of the Melbourne siege Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wataalamu wa mabomu wakiwasili eneo hilo

Polisi nchini Australia wanakichukulia kuwa kisa cha ugaidi mjini Melbourne, ambapo mtu mmoja mweye silaha aliuawa.

Polisi waliokuwa wamejihami vikali waliwasili katika nyumba moja siku ya Jumatatu baada ya ripoti za kutokea mlipuko na kupata kuwa tayari mwanamume mmoja alikuwa amekufa.

Mwanamume meingine Yacqub Khayre, alikuwa na bundukia mkoni huku akimshikilia mwnanamke mmoja ndani ya nyumba kinyume na matakwa yake,

Khayre, 29 alipigia kituo kimoja cha habari wakati huo na kusema kuwa alichukua hatua hiyo kwa jina la Islamic State.

Mtandao wa habari wa kundi la Islamic State ulisema kuwa liliendesha shambulizi hilo, lakini polisi wanasema kuwa hakuna ushahidi kuwa lilikuwa na ushikinao na Khayre.

Polisi watatu walijeruhiwa baada ya kukabiliana na Khayre ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi.

Mateka aliyekuwa akimshikilia aliokolewa bila majeraha.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Yacqub Khayre akiwa mahakamani mwaka 2010

Mada zinazohusiana