Vifo vya zaidi ya paka 200 vyazua hofu Ufaransa

paka
Image caption Paka

Kijiji kimoja cha starehe kilicho kusini mwa Ufaransa kimekumbwa na wasi wasi baada ya zaidi ya paka 200 wa kurandaranda na wa kufugwa kufa ndani ya mwezi mmoja baada ya kula sumu.

Kisa hicho kimetokea eneo la Saint Pierre la Mer kilomita 90 kutoka Kusini magharibi mwa Montpellier.

Chama cha kuwalinda wanyama kimepokea simu nyingi kufuatia kisa hicho.

Wanyama wengine na hata ndege nao walikufa baada ya kula sumu, huku kukiwa na hofu kuwa watoto huenda nao wakaila.

Chama cha paka wa kurandaranda kimeripoti matukio hayo kwa polisi kwa matumaini kuwa uchunguzi utafanywa.

"Tuna hofu kuwa mtota anawewa kuila sumu hii," mwanakijiji mmoja mwenye hofu alisema.

Image caption Kisa hicho kimetokea eneo la Saint Pierre la Mer