Balozi wa Marekani ajiuzulu kufuatia sera za Trump

David Rank (kulia) Haki miliki ya picha Reuters
Image caption David Rank (kulia)

Mwanadiplomasia wa cheo cha juu wa Marekani nchini China amejiuzulu kwa madai kuwa hakukubaliana na sera za mabadiliko ya hali ya hewa za Rais Donald Trump.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ilisema kuwa naibu Balozi David Rank alijizulu.

Vyombo vya habari nchini Marekani vilisema kuwa Bwana Rank alijiuzulu kufuatia tangazo la Trump wiki iliyopita kuwa Marekani ilikuwa inajiondoa kutoka kwa makubaliano ya Paris.

Hatua hiyo ambayo Trump alisema kuwa itasaidia kulinda uchumi wa Marekani ilizua hisia tofauti kote duniani.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ilisema katika taarifa kuwa bwana Rank alifanya uamuzi wa kibinafsi.

Bwana Rank ambaye aliteuliwa Januari mwaka 2016 alikuwa mwadiplomasia mkuu wa Marekani nchini China kwa kuwa alikuwa kaimu Balozi. Terry Branstand ambaye aliteuliwa na Trump atachukua wadhifa huo.

Rank alianza kutumikia wadhifa huo mwaka 1990 na ameshatumikia nchini Afghanistan, Taiwan, Ugikiri na Mauritius.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii