Waasi nchini Ufilipino wamejiwekea hifadhi kubwa ya chakula na silaha

Nyumba hii iliyoko mjini Marawi, Ufilipino inafuka moshi baada ya kulipuliwa na bomu kutoka angani
Image caption Nyumba hii iliyoko mjini Marawi, Ufilipino inafuka moshi baada ya kulipuliwa na bomu kutoka angani

Wapiganaji wa kiislamu ambao wamesambaratisha kabisa shughuli katika mji wa Marawi kusini mwa Ufilipino, wamejiandaa ipasavyo kuendelea kuushikilia mji huo.

Hayo ni kwa mjibu wa wakuu nchini Ufilipino.

Kwa majuma mawili sasa, wanajeshi wa nchi hiyo wanapambana na waasi hao, ili kuwaondoa kabisa katika mji huo na viunga vyake.

Inasemekana kuwa wanamgambo hao wamejificha ndani ya vichuguu na majumba ya chini ya ardhi, huku wakiwa na hifadhi kubwa ya chakula na silaha.

Image caption Ramani ya Ufilipino ikionyesha mji wa Marawi

Mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu 170, wkiwemo raia 20, huku zaidi ya wakazi 180,00 wamekimbia maskani yao.

Mamia kadhaa ya raia wanaaminika kukwama, wakiwa na hifadhi ndogo zaidi ya chakula.

Serikali ya nchi hiyo ambayo imekuwa ikitekeleza mashambulia ya angani, awali ilidai "kufaulu" katika mapambano hayo, lakini hawajafaulu kuchukua kabisa udhibiti wa mji huo.

Afisa mmoja mkuu wa kijeshi amewaambia wanahabari kuwa jeshi linaamini wanamgambo hao wamejificha, katika mtandao mpana wa mashimo chini ya ardhi, yaliyojengwa miaka kadhaa iliyopita.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bendera ya Islamic State imeonekana katika mji wa Marawi

"Kuna mashimo mengi na mahandaki chini ya ardhi na kwenye orofa ya chini ya majumba hata bomu lenye uzito wa kilo 500, haziowezi kuziharibu," amesema Meja Jenerali Carlito Galvez, ambaye ni Jemedari mkuu anayeongoza operesheni hiyo katika eneo hilo lililoko magharibi mwa Mindanao.

Serikali ya Rais Duterte na jeshi la nchi hiyo inakisia kuwa wanamgambo ambao wangali mjini Marawi wana kisiwa kuwa kati ya 40- 200.

Katika taarifa nyingine:

Serikali ya Ufilipino imekanusha madai kuwa, wanajeshi wake wanapora mali mjini Marawi, huku ikisema kuwa vikosi vya jeshi vilipeana kwa serikali zaidi ya Pesos ya Ufilipino zipatazo milioni 79 kama dola milioni 1 nukta 2, taslimu na hundi, ambayo ilipatikana ndani ya mojawepo ya nyumba ambayo ilikuwa ikitumika na wanamgambo hao.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wengi wa wakaazi 200,000 wa mji wa Marawiwamekimbia makabiliano hayo, huku wakitafuta hifadhi katika kambi za muda

Rais Rodrigo Duterte, ameongeza zawadi aliyotoa kwa yeyote atakayetoa taarifa aliko kinara mkuu wa kundi la wanamgambo hao Bw. Isnilon Hapilon na Maute brothers, ya kima cha pesos milioni 27.4 au dola Milioni 5 za Kimarekani.

Kundi la The Maute, linajulikana kwa jina hilo baada ya waasisi wake na viongozi wake Abdullah na Omar Maute.

Marekani imewapa wanajeshi wa Ufilipino bunduki za rashasha na silaha zinazorusha mbali magrunedi, ambazo zitatumika kukabiliana na waasi hao wa I-S mjini Marawi.