Safari ya kuufikia mti mrefu zaidi Afrika nchini Tanzania

Safari ya kuufikia mti mrefu zaidi Afrika nchini Tanzania

Ili kufika katika eneo la Mrusungu ambapo ndipo ulipo mti huo mrefu zaidi, ni safari ya kutembea kwa mguu kwa takriban muda wa saa nne kwenda na kurudi kwa kupita katika milima, mabonde, mito na makorongo.

Charles Ngendo ambaye ni mhifadhi wa utalii katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro amesema hifadhi inatarajia kuboresha miundombinu ya kufika katika mti huo ili kuwawezesha watalii kwenda kwani miundombinu ya sasa hivi sio rafiki kwa utalii.