Marekani na Wakurdi wavamia ngome ya I-S Mjini Raqqa

Wanajeshi wa Syrian Democratic Forces, wamekuwa wakiusogea mji wa Raqqa taratibu tangu mwisho wa mwaka jana Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa Syrian Democratic Forces, wamekuwa wakiusogea mji wa Raqqa taratibu tangu mwisho wa mwaka jana

Baada ya kisa kibaya cha milipuko mikubwa ya mabomu kutoka kwa ndege za wanajeshi wa muungano wakiongozwa na Marekani, SDF inasema kuwa, wapiganaji wake sasa wameingia katika Wilaya zilizoko katika maeneo ya kazkazini na mashariki mwa mji wa Raqqa.

Wameeleza operesheni hiyo kama mwanzo wa vita vikuu vya kuukomboa mji wa Raqqa kutoka mikononi mwa wanamgambo wa Islamic State-- ambao wameutumia kama makao yao makuu nchini Syria tangu mwaka 2014.

Operesheni ya kuukomboa mji wa Raqqa yaanza

Uturuki na Marekani kushambulia ngome ya IS Syria

Uturuki yataka balozi wa Marekani aondolowe Syria

Wanajeshi wa Syrian Democratic Forces, (SDF) wamezingira mji huo katika maeneo ya Kaskazini, magharibi na mashariki, lakini wanaonekana wameacha wazi meneo ya Kusini ili wapiganaji wa I-S pamoja na raia wakimbie.

Image caption Ramani ya mashariki ya kati

Kamanda mkuu wa majeshi ya muungano chini ya Marekani dhidi ya I-S, Luteni Jenerali Steve Townsend, amesema kuwa mapigano hayo yatakuwa magumu na yatachukua muda mrefu, lakini hilo litawapa pigo kubwa mno kwa mawazo ya wana- I-S, ambao wanapania kuunda utawala wao.

Operesheni hii imekuwa ikisubiriwa kwa muda, kwani wanajeshi wa SDF , wamekuwa wakiusogelea mji wa Raqqa tangu Novemba mwaka jana, na hali ikawa kanganyifu mno, hasa baada ya Uturuki hasa, ilipowaona wapiganaji wa Kikurdi kuwa sawa na wapiganaji wa I-S.

Hata hivyo jirani ya Syria, Uturuki kupitia kwa waziri mkuu wake Binali Yilderim, ameilaani Marekani huku akisema inawahami na kufanya kazi na kundi la kigaidi.

Amezungumza na waandishi habari Jumanne jioni huku akisema kuwa "huwezi kutumia kundi moja la kigaidi kuzima lingine" huku akimaanisha kuwa, kundi hilo la SDF linaloongozwa na Wakurdi ni la kigaidi na halifai kupewa silaha na Marekani ili kupambana na wanamgambo wa Islamic State.