Aliyemchochea mpenzi ajiue ili ahurumiwe amefunguliwa mashtaka Marekani

Michelle Carter Haki miliki ya picha WCVB
Image caption Bi Michelle Carter sasa na miaka 20

Mwanamke mmoja wa miaka 20 raia wa Marekani ,ambaye mpenziwe alijiuaa miaka mitatua iliyopiya baada ya madai kuwa alimshawishi ajiue amefunguliwa mashtaka.

Michelle Carter ameshtakiwa kwa mauaji kwa na wajibu wake katika kujiua kwa Conrad Roy III.

Waendesha mashtaka wanasema kuwa Bi Carter alisababisha kijana huyo wa umri wa miaka 18 kujiwa ili apate kuhurumiwa.

"Unaitajia kufanya hivyo," Bi carter alimuandikia ujumbe asubuhi ya tarehe 12 Julai.

"Uko tayari na umejiandaa, kileanahitaji kufanya ni kuwakisha jenereta na utakuwa huru na raha." Bi Carter aliandika.

Haki miliki ya picha WCVB
Image caption Bwana Roy

Bwana Roy alipatikana akiwa amekufa kutokana na sumu ya gesi ya Carbon Monoxide ndani ya gari lake huko Fairhaven, Masachusetts tarehe 13 mwezi Julai mwaka 2014.

Baada ya kifo chake Bi Carter alichangisha pesa na kufanya hamasishoa kuhusu afya ya akili.

Mamake Roy aliiambia mahakama siku ya Jumanne kuwa alifikiri kuwa mwanawe alikuwa na mzongo wa mawazo.

Wakati wa soku ya kifo chake bwnaa Roy alienda eneo moja la kisrarehe huko masachusetts akiandamana na mamake na pia dadake zake.

Haki miliki ya picha Facebook
Image caption Bi Carter (kushoto) na Roy r

Hapo aliwanunulia dada zake aiskrimu na kuzungumza masuala kadha ikiwemo ufadhili wa masomo alioupata na mipango mingine ya siku za usoni.

Hata hivyo wakili wa Bi Carter aliiambia mahakam kuiwa Carter alikuwa amemzuia mpenzi wake kujiua mara kadha.

Hivi majuzi nakala fulani zilionyesha kuwa bwana Roy alikuwa amejaribu kujiua mara kadha.