Pesa zaongezeka na kutoweka kimiujiza kutoka akaunti za benki Ufilipino

A casino financier wearing rings and with painted fingernails Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Pesa zaongezeka na kutoweka kimiujiza kutoka akauntii za benki Ufilipino

Benki ya Philippines Islands BPI inasema kuwa tatazo kubwa la mtandao limesababisha pesa kutoweka na pia kuongezeka kwa akaunti za wateja nchini Ufilipino

Tatizo hilo lilisababisha kutoweka kwa maelfu ya pesa za ufilipino, huku baadhi ya watu wakiripoti kuwa walipoteza pesa zote.

Mkurugenzi mkuu wa BPI Cezar Consing, aliomba msamaha siku ya Jumatano wakati wa mahojiano na kituo kimoja cha runinga.

"Huu sio ukukuzua, hili ni tatizo la ndani," alisema.

Walio na qkaunti katika benki hiyo waliandika katika mitandao ya kijamii wakisema kuwa walipoteza hadi doa 80.

Benki ya BPI ilisema kuwa baadhi ya wateja walishuhudia akaunti zao zikipoteza pesa mara mbuili au zikiongezwa pesa mara dufu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pesa zaongezeka na kutoweka kimiujiza kutoka akauntii za benki Ufilipino