Majaji Brazil kupiga kura ya kumuondoa Rais Temer

Maafisa wa polisi wakilinda mahakama kuu ya kikatiba, mahali kesi dhidi ya Rais wa Brazil Michel Temer' inasikizwa Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maafisa wa polisi wakilinda mahakama kuu ya kikatiba, mahali kesi dhidi ya Rais wa Brazil Michel Temer' inasikizwa

Mahakama kuu ya kikatiba nchini Brazil, imerejelea vikao vyake katika kesi ya kumuondoa Rais wa nchi hiyo, Michel Temer.

Mahakama hiyo ambayo imepewa majukumu ya kusimamia shughuli za uchaguzi mkuu, inachunguza iwapo pesa haramu zilitumika katika kampeini na hatimaye ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2014.

Huo ndio uchaguzi mkuu ambao Bi Dilma Rousseff alishinda, huku Bwana Temer akiwa mgombea mwenza.

Bi Roussef, alingolewa madarakani baada ya kupigiwa kura isiyokuwa na imani na mahala pake pakachukuliwa na Bw. Temer.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Temer aliyechukua mahala pa Bi Dilma Rousseff - huenda naye akafuata mkondo huo?

Bi Roussef, alishutumiwa kwa makosa ya kuhamisha hazina ya fedha za serikali kutoka akaunti moja hadi nyingine.

Kama matokeo Bw. Temer akachukua kiti cha Urais wa Brazil mnamo Agosti mwaka 2016.

Hata hivyo, kesi hii, ambayo ilisimamishwa kwa muda mwezi Aprili, itafutilia mbali matokeo nzima ya uchaguzi mkuu mwaka 2014, hii ikiwa na maana kuwa ataondolewa ofisini.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Waandamanaji mjini Sao Paulo wamekuwa wakishinikiza kuondolewa madarakani kwa Bw. Temer

Ni kwa njia ipi majaji wataamua?

Majaji 7 wanachunguza kesi hiyo, ambayo imegawanywa kwa vikao vinne tofauti: Jumanne jioni, Jumatano Jioni na vikao vingine viwili siku ya Alhamisi.

Ikiwa majaji wataamua kuwa kampeini za uchaguzi mkuu zilipata ufadhili wa pesa haramu, bila shaka uchaguzi huo utafutiliwa mbali na Rais Temer atatimuliwa kazini.