Tufani kali yawauwa watu 8 Afrika Kusini

Alex De Kock alipiga picha hii akitazama kimbunga hicho kutoka kilima cha Signal Hill mjini Cape Town Haki miliki ya picha Image Copyright
Image caption Alex De Kock alipiga picha hii akitazama kimbunga hicho kutoka kilima cha Signal Hill mjini Cape Town

Watu 8 wamefariki baada ya kimbunga kikali kugonga mji wa Cape Town, Afrika Kusini; upepo mkali ambao vyombo vya Habari vya Afrika Kusini, vimeutaja kama "mama wa vimbunga vyote".

Miongoni waliokufa ni watu wanne wa familia moja, ambao walifariki baada ya kuteketea pale radi ilipopiga maskani yao.

Maafisa wa serikali wamesema.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Windsurfer Jake Kolnik arushwa na tufani hiyo kali

Maelfu ya watu wameachwa bila makao.

Taasisi zote za elimu zikiwemo vyuo vikuu vimefungwa, huku paa za nyumba na zikifumuliwa na upepo huo mkali.

Watu wasafiri kilomita 6 kutafuta choo Afrika Kusini

Raia 116 wa Nigeria wameuawa Afrika Kusini

Manusura wametafutiwa makao mapya mahala salama.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watabiri wa hali ya hewa wanaonya kuwa mvua kubwa itakayonyesha itasababisha mafuriko

Kimbunga hicho kinagonga baada ya kumalizika kwa ukame mkali wa karne kulikumba taifa hilo.