Uchaguzi mkuu Uingereza: Upigaji kura waanza

Polling station

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kituo cha kupigia kura

Mamilioni ya watu leo wanapiga kura kwenye uchaguzi mkuu nchini Uingereza.

Shughuli za upigaji tayari zimeanza wakati zaidi ya vituo 40,000 vikiwa vimefunguliwa kote nchini.

Jumla ya wabunge 650 watachaguliwa huku takriban watu milioni 46.9 wakiwa wamejiandikisa kupiga kura.

Ni ongezekao kutoka uchaguzi wa mwaka 2015 wakati wapiga kura milioni 46.4 walikuwa wamejiandikisha.

Kura zingine tayari zimepigwa kupitia kwa posta ambayo ilichukua asilimia 16.4 wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015.

Vituo vingi vya kupigia kura viko shuleni na katika vituo vya huduma za kijamii.

Matokeo ya viti kadha yanatarajiwa kutangazwa ifikapo usiku wa manane, huku matokeo ya mwisho yakitarajiwa kutangazwa Ijumaa mchana.

Chanzo cha picha, JEFF OVERS

Maelezo ya picha,

David Dimbleby ataongoza matangazo ya runinga BBC