Alama ya SOS huenda ikapata ufumbuzi Australia

Alama hiyo iligunduliwa na rubani wa helikopita mwezi uliopita Haki miliki ya picha WA Police
Image caption Alama hiyo ya SOS iligunduliwa na rubani wa helikopita mwezi uliopita

Polisi wanasema kuwa wamegundua yule aliacha alama ya SOS iliyotengenezwa kwa mawe katika eneo moja la mbali Magharibi mwa Australia.

Alama hiyo iligunduliwa na rubani wa helikopita mwezi uliopita na kuzua hofu kuwa mtu au watu huenda wasijulikane walipo.

Polisi sasa wanaamini kuwa ilikuwa ni alama ya kuomba msaada iliyoachwa na mwanamume na mwanamke ambao walikwama eneo hilo mwaka 2013.

Wanasema kuwa walijulishwa na ndugu ya mwanamume huyo ambaye alisoma taarafa hiyo kwenye BBC.

Image caption Swift Bay

Mwanamume huyo anayefahamika kama John anasema kuwa nduguye na mwenzake wa kike walikuwa kwenye mashua ambayo ilikuwa eneo lililo umbali wa kilomita 500 kutoka mji wa Broome mwaka 2013.

Wawili hao walichukua chombo kidogo kutoka eneo hilo ambacho wakati mmoja kilishambuliwa na mamba lakini wakafanikiwa kufika ufukweni wakiwa salama na kujenga alama hiyo ya SOS.

Afisa mmoja alisema kuwa waliishi kwa kula chakula kidogo na kunywa maji na baada wakaokolewa na mashua iliyokuwa inapita.