Faru amuua mtunza mazingira Rwanda

Faru amuua mtunza mazingira Rwanda Haki miliki ya picha Huw Evans picture agency
Image caption Faru amuua mtunza mazingira Rwanda

Mtunza mmoja wa mazingira ambaye alikuwa akisadia kuwapeleka Faru nchini Rwanda ameuawa na mmoja wa wanyama hao.

Shirika lililoandaa shughuli hiyo la African Parks, lilisema kuwa Krisztian Gyongyi, aliuwawa na Faru, katika mbuga ya taifa ya Akagera alipokuwa akiwafuatilia Faru hao.

Lakini taarifa hiyo haijasema kwa kina jinsi aliuwawa.

Mkurugenzi wa Shrika la Africa Parks Peter Fearnhead, alisema kuwa bwana Gyongyi alikuwa mtu muhimu kawarejesha Faru hao weusi na alikuwa eneo hilo kuwapa mafunzo walinzi wa mbuga jinsi ya kuwafuatilia na kuwalinda Faru

Faru hao walisafirishwa kutoka Afrika Kusini kuenda Rwanda mwezi uliopita.